Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Tafutwa
Wali Ur Rehman
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Sehemu ya kuzaliwa : Waziristan Kusini, Pakistan
Nywele : Mweusi
Macho : Kahawia
Rangi : Zeituni
Jinsia : Mwanamme
Utaifa : Raia wa Pakistan
Sifa : Ndevu kamili, masharubu
Hadhi : Aliyejifisha

Wali Ur Rehman anashika nafasi ya pili katika uongozi na kiongozi wa mikakati ya kijeshi katika kundi la Tehrik-e- Taliban Pakistan (TTP) Anaongoza wanachama wa TTP. Ameshiriki katika mashambulizi ya kuvuka mpaka katika Afghanistan dhidi ya maafisa wa jeshi la Marekani na NATO, na anatafutwa kuhusiana na kuhusika kwake katika mauaji ya raia saba wa marekani Desemba 30, 2009, katika kituo cha Forward Operating Base Chapman mjini Khost, Afghanistan

Lengo la kimsingi la TTP ni kulazimisha kuondolewa kwa majeshi ya Pakistan kutoka eneo la FATA la Pakistan, ambalo liko kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan; kufukuza maslahi ya magharibi kutoka Pakistan; na kuanzisha utawala wa Sharia- au sheria za Kiislamu—katika maeneo ya kikabila.

TTP limekuwa na majukumu yanayosemekana, katika, au kuwa na wajibu wa vitendo kadhaa vya utumiaji nguvu, kukiwa pamoja na shambulio la bomu la Septemba 2008 katika hoteli ya Marriott mjini Islamabad, ambalo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na kujeruhiwa kwa wengine 300, kukiwemo Wamarekani kadhaa. Mashambulio haya mara nyingi yaliratibiwa na waasi wengine au makundi ya kigaidi, kukiwa pamoja na Taliban na al-Qaeda.

TTP linaendelea kupanga na kufanya mashambulio dhidi ya maslahi ya Marekani kutoka eneo la FATA. Hivi karibuni, TTP limedai dhamana ya kuhusika na shambulio la bomu ambalo halikufanikiwa la Times Square mjini New York, Mei 1 2010.

Click here to listen to a Public Service Announcement about this terrorist