Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Tafutwa
Jamal Saeed Abdul Rahim
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Tarehe ya Kuzaliwa : Septemba 5, 1965
Sehemu ya kuzaliwa : Lebanon
Urefu : 5’9“
Uzito : Pauni 154 (kg70)
Nywele : Kahawia
Macho : Nyeusi
Rangi : Mzungu
Jinsia : Mwanaume
Utaifa : Mpalestina
Hadhi : Anatafutwa
Majina bandia : Ali al-Jassem Fahd, Jamal Saeed Abdulrahim, Fahad Ali al-Jasseen, Ismael, Fahad Jamal Saeed Abdul Rahim anatafutwa

Kuhusiana na utekaji nyara wa Septemba 5, 1986 wa ndege ya Pan Am 73 ikiwa ardhini mjini Karachi, Pakistan. Mtu huyu aliyetajwa hapo juu amefunguliwa mashtaka yafuatayo:

Njama za kufanya uhalifu dhidi ya Marekani; njama za kuwaua raia wa Marekani nje ya Marekani; mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; jaribio la kuwaua raia wa Marekani nje ya Marekani; kusababisha madhara makubwa ya kimwili kwa raia wa Marekani nje ya Marekani; utekaji nyara; kutumia silaha wakati wa kitendo cha uhalifu cha kutumia nguvu; kuweka vifaa vya uharibifu kwenye ndege; kufanya kitendo cha kutumia nguvu dhidi ya mtu kwenye ndege; uharamia wa ndege; uharibifu wa nia mbaya kwenye ndege; na kusaidia na kuwezesha uhalifu.

Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki, Jamal Saeed Abdul Rahim, Muhammad Abdullah Khalil Hussain ar-Rahayyal, na Muhammad Ahmed al-Munawar wamefunguliwa mashtaka katika mahakama ya District of Columbia kwa jukumu lao katika utekaji nyara wa ndege ya Pan Am 73 tarehe 5 Septemba, 1986 ikiwa ardhini mjini Karachi, Pakistan. Baada ya kuishikilia ndege na abiria wake na wafanyakazi 379, wakiwemo raia wa marekani wasiopungua 78, kwa karibu saa 16, watekaji nyara walianza kushambulia abiria kiholela, na kusababisha vifo vya abiria wasiopungua 20 na kujeruhi vibaya wengine zaidi ya 100. Watu hawa wanaaminika kuwa wafuasi wa Shirika la Abu Nidal, shirika la mfumo wa magaidi wa kimataifa.

Click here to listen to a Public Service Announcement about this terrorist