Maswali yanayoulizwa mara nyingi
Je unaweza kutoa taarifa kuhusu Mpango wa Tuzo kwa Haki (RFJ)?
Tuzo zinazotolewa zinatangazwa vipi?
Habari zipi unazitoa kuhusu malipo ya tuzo?
Je unaweza kutoa maelezo kuhusu malipo bayana ya tuzo?
Tunaweza kuhakikisha vipi kwamba mmeshalipa tuzo kama hamtoi maelezo dhahiri?
Kitu gani unapaswa kufanya ili upate tuzo? Aina gani ya habari unazoziangalia?
Je kiwango cha malipo ya tuzo kinaamuliwa vipi?
Unaweza kutoa maelezo kuhusu Mfuko wa Tuzo kwa Haki?
Kwa kutoa tuzo, je hushawishi watu kujichukulia sheria mkononi?
Kama ninataka kutoa habari, nawasiliana na nani?
Je unaweza kutoa taarifa kuhusu Mpango wa Tuzo kwa Haki (RFJ)?
RFJ ni kitengo kinachoshughulikia ugaidi katika Wizara ya Mambo ya Nje, kilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1984 ya kupambana na ugaidi wa kimataifa, sheria ya umma 98-533 (kipengele cha namba U.S.C. 2708). kinachosimamiwa na Idara ya Ulinzi wa Kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, lengo la RFJ ni kuwafikisha magaidi wa kimataifa mbele ya sheria ya kuzuia vitendo vya kigaidi dhidi ya Wamarekani au mali zao. Chini ya mradi huu, Waziri wa Mambo ya Nje ataidhinisha tuzo kwa habari zitakazopelekea kukamatwa au kushtakiwa mtu yoyote ambaye anapanga, anatenda au anajaribu kufanya vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya wamarekani au mali zao, ambavyo vitazuia kufanyika vitendo kama hivyo, ambavyo vitasababisha kujulikana kwa eneo aliko kiongozi wa ugaidi, au ambavyo vitavuruga ufadhili wa kifedha wa ugaidi.
RFJ inatunza orodha ya tuzo mpya zilizotolea kwenye mtandao wake: www.rewardsforjustice.net. Tuzo nyingi za RFJ ni dola zinazofikia milioni tano. Hata hivyo, tuzo zinazotolea zinaweza kuanzia chini ya dola milioni moja mpaka dola milioni 25, katika kesi kama ya Usama Bin Ladin na viongozi wengine waandamizi wa Al Qaida. kwa kuongezea, RFJ inaweza pia kulipa tuzo katika kesi ambazo hakuna tuzo za awali ambazo zimetolewa, katika hali zinazostahili.
Tangu kuanzishwa kwake, RFJ imelipa zaidi ya dola milioni 77 kwa watu binafsi zaidi ya 50 kwa habari ambazo zimepelekea kuzuia mashambulizi ya ugaidi wa kimataifa au kusaidia kuwafikisha wale waliohusika na vitendo hivyo awali.
Kuhusiana na mradi wa RFJ, vyanzo vinaweza kutoa habari ambazo zilisaidia kuzuia au kusuluhisha vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya maslahi ya Marekani na kuwafikisha mbele ya sheria magaidi hatari sana hapa duniani. Juhudi hizi zinaweza kuokoa maisha ya watu wasiokuwa na hatia.
Nchini Iraq, kwa mfano, siku 18 tu baada ya kutangazwa kwa tuzo kwa ajili ya Uday na Qusay Hussein, chanzo kiliitokeza na kutoa habari kuhusiana na mahali walipo. Mafanikio mengine yaliyotangazwa sana ni kukamatwa kwa Ramzi Yousef, mmoja wa walipuaji mabomu mwaka 1993 kwenye kituo cha biashara cha World Trade Center, ambaye aligundulika mwaka 1995, ikiwa ni matokeo ya habari zilizotolewa na chanzo kwa kuitikia tangazo la tuzo lililotolewa na RFJ.
Tuzo zinazotolewa zinatangazwa vipi?
Na mbali na tovuti ya RFJ, tunatumia mabango, vijitabu, matangazo ya malipo kwenye radio na kwenye magazeti, mtandao wa internet, na kwenye sehemu yoyote muafaka kusaidia kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Marekani.
Habari zipi unazitoa kuhusu malipo ya tuzo?
Kiungo muhimu cha mradi huu ni kwamba tunahakikisha majibu kwa kampeni yetu ya tuzo yanakuwa siri kubwa. Na lililo muhimu zaidi, hatutoi majina ya watu ambao wamelipwa tuzo, na kwa kawaida hatutoi hadharani maelezo yoyote kuhusu tuzo zilizolipwa. Na katika kesi za wahalifu muhimu, tunatangaza malipo ya tuzo, lakini hatutoi habari zaidi.
Je unaweza kutoa maelezo kuhusu malipo bayana ya tuzo?
Malipo makubwa yaliyotolewa hadi hivi leo ni dola milioni 30 kwa mtu mmoja ambaye alitoa habari ambazo zilipelekea kukamatwa kwa Uday na Qusay Hussein.
Kumekuwepo sherehe nne za tuzo za RFJ huko Phillipines. Tuzo ya karibuni ilikuwa June 7, 2007, na jumla ya tuzo iliyotolewa katika sherehe hiyo ilifikia dola milioni 10. Malipo ya tuzo hii ni malipo makubwa kuwahi kufanywa na RFJ nchini Phillipines tangu mradi huu ulipoanzishwa.
Tunaweza kuhakikisha vipi kwamba mmeshalipa tuzo kama hamtoi maelezo dhahiri?
Kama ilivyoelezewa, RFJ mara kwa mara inatoa matangazo kiasi kuhusu tuzo za malipo ya wahalifu muhimu. Pia tunapeleka ripoti ya siri kwa Bunge baada ya malipo kutolewa.
Kitu gani unapaswa kufanya ili upate tuzo? Aina gani ya habari unazoziangalia?
Mtu yoyote ambaye anatoa habari ambayo itatusaidia ama kuzuia au kuzuia kwa ufanisi vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya Marekani kokote hapa duniani huenda akastahili kupewa tuzo.
Ikiwa, kwa mfano, gaidi anayehusika ama katika kupanga au kutekeleza shambulizi dhidi ya Wamarekani na/ au mali zao atakamatwa au kushtakiwa kutokana na habari iliyotolewa na chanzo, chanzo hicho huenda kikastahili kupewa tuzo.
Kwa kuongezea, mtu yoyote mwenye habari kuhusiana na kujulikana au sehemu ambako yuko kiongozi wa kundi la ugaidi wa kimataifa huenda akastahili kupewa tuzo. Tuzo pia huenda zikalipwa kwa habari kuhusu mtu binafsi au kundi ambalo linasafirisha madawa ya kulevya kwa ajili ya kufadhili vitendo vya ugaidi wa kimataifa au kuchangisha fedha kugharimia au kuunga mkono kundi la kigaidi.
Hata hivyo, chini ya sheria ambayo inauhusu mpango huu, wafanyikazi wa serikali ya Marekani, majimbo, wilaya na wafanyakazi wa serikali za kigeni kwa ujumla hawawezi kushiriki katika mpango wa tuzo hii kama watatoa habari ambazo wamezipata katika shughuli zao rasmi za kazi.
Je itakuwaje kama mtu atahatarisha maisha yake kwa kutoa habari kuhusu gaidi na halafu akagundua kwamba maisha yake yako katika hatari? Je RFJ inaweza kutoa ulinzi?
Kama ilvyojadiliwa hapo juu, usiri ni nguzo ya mpango wa RFJ. RFJ itaficha jina la mtu yoyote ambaye anatoa habari kwa kuitikia mwito wa tuzo na/au ambaye amepewa malipo ya tuzo. Kwa kuongezea, kumhamisha mtu huenda kukafanyika kwa mtu na familia yake, lakini masuala haya yatatakiwa yaamuliwe kulingana na kesi kwa kesi.
Kila tuzo itakayoteuliwa itafikiriwa katika misingi ya kesi kwa kesi. Utaratibu wa malipo ya tuzo ni kama ufuatavyo:
Kila idaraya Marekani inayofanya uchunguzi, kama vie Wizara ya Ulinzi au FBI, au ubalozi wa Marekani nje, lazima kwanza wateue mtu kwa tuzo hii. Na kamati ya idara itafanya tathmini ya kina kuhusu habari iliyotolewa. Ikiwa kamati ya Idara inayohusika na utoaji wa tuzo itaamini kuwa mtu huyo anastahili kupewa tuzo, itapeleka mapendekezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa ajili ya kuidhinisha tuzo hiyo.
Mapendekezo ya kamati hata hivyo, si ya mwisho. Waziri wa Mambo ya Nje ana maamuzi ya mwisho kuhusu kuidhinishwa kwa tuzo itakayotolewa, na anaweza kubadili fungu la tuzo, kwa kuzingatia misingi ya sheria.
Kama kuna suala la kihalifu katika jambo hili, Waziri atapeleka mapendekezo kwa Waziri wa Sheria kabla ya tuzo kutolewa.
Je kiwango cha malipo ya tuzo kinaamuliwa vipi?
Kiwango cha malipo ya tuzo kitatolewa kulingana na vigezo kadhaa, ikiwa pamoja na ukubwa wa kitisho ambacho kinatolewa na gaidi, ukubwa wa hatari au madhara kwa Wamarekani au mali, ubora wa habari zilizotolewa, na hatari inayomkabili mtoaji habari na familia yake, pamoja na kiwango cha ushirikiano wa mtu huyo katika uchunguzi au kesi.
Unaweza kutoa maelezo kuhusu Mfuko wa Tuzo kwa Haki?
Mfuko wa Tuzo kwa haki ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida kulingana na kipengele 501(c)(3) taasisi ya hisani ambayo ina uhusiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Mradi wa Tuzo kwa Haki upo kwa lengo la kuchangisha na kupata michango binafsi kwa ajili ya matumizi katika kutambua na kuwakamata wanaotaka kutenda ugaidi ndani ya Marekani na nje. Mfuko wa Tuzo kwa Haki ulianzishwa na kusimamiwa na kundi na Wamarekani. Kundi hilo liliifuata Wizara ya Mambo ya Nje muda mfupi baada ya mashambulizi ya September 11 na kuomba kudhinishwa kuchangisha fedha kupitia michango kutoka kwa umma kwa ujumla ili kuisaidia RFJ. Tulilitathmini hili pendekezo na kuunga mkono juhudi za Mfuko wa Tuzo kwa Haki. Maswali ya ziada lazima yaelekezwe kwenye mfuko huo katika mtandao www.rewardsfund.org.
Kwa kutoa tuzo, je hushawishi watu kujichukulia sheria mkononi?
Hatushawishi watu wajichukulie sheria mikononi na watu wengine kutoka taasisi binafsi waanze kuwatafuta na kuwakamata magaidi; badala yake, RFJ inatoa tuzo kwa habari ambazo zitazisaidia mamlaka za serikali kuwapata na kuwakamata watu kama hao.
Kama ninataka kutoa habari, nawasiliana na nani?
Watu wenye habari lazima wawasiliane na Ofisi ya Usalama katika eneo katika ubalozi wa Marekani au Ubalozi mdogo, FBI au kutuma habari sehemu hii:
Anwani ya Posta: RFJ, Washington DC 20522-0303, USA Namba ya Simu: 1-800-US-REWARDS. Barua Pepe: RFJ@state.gov
Ningependa kuomba ruhusa kutumia picha zifuatazo kutoka kwenye mtandao wenu katika kuwasilisha habari hizi au kuchapisha.
Isipokuwa kama kuna suala la haki miliki, habari katika mtandao huu ni kwa ajili ya umma kuangalia na zinaweza kunakiliwa, kuchapishwa au vinginevyo kutumiwa bila ya ruhusa ya RFJ. Tunaomba RFJ itajwe kuwa ni chanzo cha habari na kwamba picha yoyote lazima ielezewe ilikopatikana au kutajwa imepigwa na nani au mwandishi au RFJ kama inavyostahili.
Kama haki miliki imeelezewa kwenye picha, mchoro au kitu chochote, ruhusa ya kunakili vitu hivi lazima itolewe kutoka kwa chanzo cha awali. Kwa kuongezea, lazima ieleweke kuwa kuna kipengele cha kihalifu, 18 U.S.C> 713, ambacho kinazuia matumizi ya nembo ya Marekani chini ya misingi hiyo iliyoelezewa katika kipengele hicho; kwahiyo, tunapendekeza kwamba uwasiliane na afisa mhusika kabla ya kutumia nembo hiyo kwa njia yoyote ile.
