Anayetafutwa
Ahmed Mohamed Hamed Ali
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5
Sehemu Alikozaliwa : Misri
Urefu : Mwenye urefu wa kiasi cha futi 5na inchi 6 mpaka futi 5 inchi 8 (sentimeta 168 - 173)
Umbile : Wastani
Nywele : Mweusi
Macho : Mweusi
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Raia wa Misri
Majina Mengine : Shuaib, Abu Islam al-Surir, Ahmed Ahmed, Ahmed The Egyptian, Ahmed Hemed, Hamed Ali, Ahmed Shieb, Abu Islam, Ahmed Mohammed Ali, Ahmed Hamed, Ahmed Mohammed Abdurehman, Abu Khadiijah, Abu Fatima, Ahmad al-Masri
Ahmed Mohamed Hamed huenda amesomea kilimo na inawezeka amefanya kazi katika fani hiyo. Ameshtakiwa kwa tuhuma za kuhusika kulipua mabomu ubalozi wa Marekani Dar es Salaam,Tanzania na Nairobi, Kenya mwaka 1998, August 7.
Mtu aliye orodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:
Njama za kuua raia wa Marekani, kufanya mauaji, kuharibu majengo na mali za Marekani, na kuharibu vituo vya huduma za ulinzi wa Marekani.
Usama bin Ladin, Ayman al-Zawahiri, Fazul Abdullah Mohammed, Fahid Mohammed Ally Msalam, Sheikh Ahmed Salim Swedan, Abdullah Ahmed Abdullah, Saif al-Adel, Anas al-Liby, Ahmed Mohamed Hamed Ali, na wengine tayari wako chini ya ulinzi na wanaaminika kuhusika na ulipuaji mabomu kwenye Ubalozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya hapo August 7, 1998. Ulipuaji balozi ulisababisha vifo vya raia 224 na kujeruhi wengine elfu tano. Magaidi hawa wanaaminika ni wanachama wa Al-Qaida, mtandao wa kimataifa wa ugaidi unaoongozwa na Usama bin Ladin.

