Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Usama bin Ladin
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 25


Tarehe ya Kuzaliwa : 1957
Sehemu Alikozaliwa : Saudi Arabia
Urefu : Futi 6 inchi 4 - futi 6 inchi 6 (sentimeta 193 - 198)
Uzito : Uzito paundi 160 (kilo 71)
Nywele : Kahawia
Macho : Kahawia
Rangi : Zeituni
Jinsia : Mwanamme
Utaifa : Raia wa Saudi Arabia
Tabia : Ana Sharafa, masharubu; anatembea na fimbo.
Cheo : Mtoro
Majina Mengine : Usama bin Muhammad bin Ladin, Shaykh Usama bin Ladin, Mwana mfalme, Mkuu, Abu Abdalla, Mujahid Shaykh, Hajj, Mkurugenzi

Usama bin Ladin anatafutwa kuhusiana na mashambulizi ya Septemba 11, 2001 kwenye majengo ya World Trade Center na Pentagon na ulipuaji mabomu wa August 7, 1998 kwenye Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya.

Mtu aliye orodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; njama za mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; na mashambulizi kwenye vituo vya serikali kuu yaliyosababisha vifo.

Usama bin Ladin, Ayman al-Zawahiri, Fazul Abdullah Mohammed, Fahid Mohammed Ally Msalam, Sheikh Ahmed Salim Swedan, Abdullah Ahmed Abdullah, Saif al-Adel, Anas al-Liby, Ahmed Mohamed Hamed Ali, na wengine tayari wako chini ya ulinzi na wanaaminika kuhusika na ulipuaji mabomu kwenye Ubalozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya hapo August 7, 1998. Ulipuaji balozi ulisababisha vifo vya raia 224 na kujeruhi wengine elfu tano. Magaidi hawa wanaaminika ni wanachama wa Al-Qaida, mtandao wa kimataifa wa ugaidi unaoongozwa na Usama bin Ladin.