Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Ahmad Ibrahim al-Mughassill
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Tarehe ya Kuzaliwa : Juni 26, 1967
Sehemu Alikozaliwa : Saudi Arabia
Urefu : Futi 5 inchi 4 (sentimeta 163)
Nywele : Mweusi
Macho : Kahawia
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Raia wa Saudi Arabia
Majina Mengine : Abu Omran

Juni 25 mwaka 1996, wanachama wa Saudi Hizballah walifanya mashambulizi ya ugaidi kwenye jengo la gorofa za Khobar karibu na Dhahran, Saudi Arabia. Muda huo jengo hilo lilikua likitumika kama makazi ya wafanyakazi wa jeshi la Marekani. Magaidi waliendesha gari la kubebea mafuta lililojazwa mabomu kwenye maegesho ya gari na kuliripua, wakiharibu jengo la ujirani. Shambulizi liliua wanajeshi 19 wa Marekani na raia mmoja wa Saudi, na kujeruhi 372 wa mataifa mengine mbalimbali.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa katika mahakama ya Eastern District ya Virginia mwaka 1996 Juni 25, kwa kuripua bomu jengo la ghorofa za Khobar huko Dharran, Saudi Arabia.

Mtu aliye orodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Njama ya kuwaua raia wa Marekani , njama ya kufanya mauaji, njama ya kutumi silaha za maangamizi dhidi ya raia wa Marekani, njama za kuharibu rasilimali ya Marekani. Njama ya kushambulia huduma za ulinzi wa kimataifa, kuripua mabomu na kusababisha vifo, kutumia silaha za uharibifu mkubwa dhidi ya raia wa Marekani, mauaji kwa kutumia mbinu za uharibifu wakati wa uhalifu, Mauaji ya wafanyakazi wa serikali, na kujaribu kuua wafanyakazi wa serikali.